CPB YATANGAZA FURSA KWA WAKULIMA, WAFANYABIASHARA WA MAZAO , NA IMMACULATE RUZIKA-CPB.

CPB YATANGAZA FURSA KWA WAKULIMA, WAFANYABIASHARA WA MAZAO , NA IMMACULATE RUZIKA-CPB. MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Salum Awadh ametangaza fursa mbalimbali zinazotolewa na CPB kwa wakulima na wafanyabiashara wa Mazao hapa nchini.   Aidha Awadh alitaja baadhi ya fursa zinazotolewa na CPB ni pamoja kilimo cha mkataba ambacho kitaanzia na hekali 1000 na kuendelea.   Akizungumza katika kikao cha wadau kilichofanyika Iringa Awadh alisema Kilimo cha mkataba CPB kitakuwa na uwezo mkubwa kutoa maelekezo na ufuatiliaji kwa urahisi.   ” Kilimo cha mkataba kitasaidia kuwa na uhakika wa wakulima watakaotuletea mazao, yatakuwa katika ubora”‘ alisema Awadh.   Mwenyekiti huyo alisema fursa zingine ni pamoja na kuhitaji Mawakala ambao wataingia nao mkataba kwaajili ya uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa CPB na kununua mazao kutoka kwa wakulima na wafanyabishara.   Awadh alisema CPB ni Shirika la Kibiashara la Serikali hivyo linafanya biashara kwa lengo la kuinua Uchumi wa Nchi lakini na mtu mmoja mmoja.   “Biashara ambayo CPB inafanya hatuwezi kumlalia mkulima au mfanyabiashara wa mazao, Sisi lengo letu, Sisi tupate na nyie mpate,alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi.   Aidha Awadh alisema CPB ina maghala ambayo hutumia kuhifadhia mazao na bidhaa zao, hivyo wanafanya pia biashara ya kuhifadhi mazao katika maghala hayo ambayo yapo katika Mikoa mbalimbali.   vilevile Mwenyekiti huyo alisema kuwa CPB pia inatafuta masoko kwa Wakulima kama wanunuaji lakini kuwatafutia wakulima na wafanyabiashara kuwa inganisha na masoko ya nje.   Aidha Awadh alisema CPB inaongezea thamani mazao kwa kuchakata mazao kama Mpunga, Mahindi, Ngano, Alizeti na Siagi kupitia Viwanda vya CPB vilivyopo katika baadhi ya Mikoa ikiwemo Iringa.