CPB Kanda ya Kati inajumuisha maeneo ya Dodoma, Singida, Tabora, Katavi na Kigoma. CPB ilipata ardhi manispaa ya Dodoma katika eneo la mbugani barabara ya Veta na eneo la Kizota (eneo la viwanda magharibi), yenye wastani wa hekta 3.7 na 1.92 mtawalia.
Ofisi kuu kanda ya kati ipo Kizota, yenye ofisi ndogo – kituo cha mauzo (POS) katika Eneo la Mbugani karibu na majengo ya bunge, ambapo mauzo na manunuzi wa mazao yanashughulikiwa.
Ofisi ya Kanda ya Kati eneo la Kizota ina kiwanda cha kisasa cha kusaga mahindi chenye uwezo wa kusindika tani 60 za mahindi kwa siku, kituo cha kusindika mafuta ya alizeti chenye uwezo wa kusindika tani 20 za alizeti kwa siku, maabara yenye vifaa vya kisasa yenye uwezo wa kufanya kazi kwa ubora ambayo huchunguza bidhaa zinazozalishwa kabla ya kupelekwa sokoni, na kantini ambayo hutoa huduma za upishi kwa jumuiya ya CPB na umma kwa ujumla.
Kanda ya kati pia ina maghala na vifaa vya kuhifadhi nafaka vyenye uwezo wa jumla ya metriki tani 32,000. Maghala yake ya vitanda yanapatikana katika vitengo sita vya tani 5,000 na kitengo kimoja cha tani 2,000. Maeneo hayo ya kuhifadhia yapo mita 300 kutoka kituo cha treni cha Dodoma na mita 200 kutoka barabara kuu ya Dodoma - Dar Es Salaam. Sehemu kituo kilipo pamoja na barabara za lami zinazozunguka kituo hiki huwezesha kwa wingi usafiri wa kwenda na kurudi, hivyo kufanya kufanya hupatikanaji na hufikiaji wa kituo hiki kuwa rahisi. Kituo pia kina nafasi kubwa ya maegesho
BIDHAA NA HUDUMA ZITOLEWAZO
Sisi ni wasambazaji wa bidhaa za kilimo, mbichi na zilizosindikwa. Tunanunua, tunaweka daraja la ubora pamoja na kuuza aina mbalimbali za mazao kama vile mahindi, maharage ya kila aina, mtama, mpunga, karanga na mazao mengine kadri inavyohitajika. Bidhaa zetu zilizosindikwa, ambazo ni pamoja na Dona bora na Sembe bora, mafuta ya alizeti ya CPB yanauzwa kwa jina la chapa NGUVU. Korosho zetu, zilizokaangwa na mbichi zinauzwa kwa jina la chapa Tan Korosho.
Pia tunauza vyakula vya mifugo kama pumba za mahindi, alizeti na mashudu ya pamba. Wilaya za Manyoni, Mpwapwa, Kongwa, Bahi, Chamwino, Chemba, Kondoa, Gairo Singida, Iramba, Itigi, Morogoro, Dar es Salaam na pamoja na wilaya za ukanda wa pwani zinahudumiwa na wasambazaji wetu.
Huduma Zetu Nyingine ni Pamoja na:
Fursa za kushirikiana na CPB kanda ya kati
-
Uwekezaji katika vifaa vya usindikaji na uhifadhi.
-
Biashara ya bidhaa za kilimo.
-
Wasafirishaji.
-
Usambazaji wa bidhaa za CPB
-
Mawakala wa bidhaa zetu
-
Wakala wa usambazaji na kusafisha
-
Usambazaji wa vifungashio
-
Huduma za uchapishaji,
-
Matangazo na mawakala wa matangazo.
"Tunawaalika wadau wenye uwezo kufanya kazi na Bodi ya Nafaka na Mazao mengine Tanzania"