CPB YA HUDHURIA MKUTANO PULSE ,MUMBAI KATIKA KUTAFUTA FURSA ZA KUUZA NJE KWA MAZAO PAMOJA NA KUJADILIANA KUANZISHA USHIRIKIANO NA CHAMA CHA KUNDE NCHINI INDIA
Majadiliano yamefanyika na mwenyekiti wa Chama cha Kunde na Nafaka cha India, Bw. Bimal Kothari, kuhusu kutia saini *MoU na CPB Majadiliano yamelenga kuanzisha ushirikiano wa kukuza na kusaidia wakulima wa kunde, wafanyabiashara na wadau wengine. Katika Kuhudhuria mkutano huo wa kimataifa wa pulses huko Mumbai ni katika kutafuta fursa za kuuza nje kwa wakulima wa TZ ili kuongeza mauzo ya nje kwenda India. TZ inazalisha 2.1m MT, huku 85% ya wakulima wakiwa na wastani wa ekari 5/mkulima. India ndiyo mzalishaji na mtumiaji mkubwa zaidi, ikiwa na upungufu wa 4m - 6m MT kila mwaka. Lengo ni kuongeza ubora wa mbegu, uhamisho wa ujuzi, na upatikanaji wa soko CPB pia inapanga kushirikiana kama mshiriki mwenza wa mkutano wa kilele wa bidhaa za kilimo na chakula mwaka huu nchini Tz, ili kufungua masoko.