CPB KANDA YA ZIWA YAINGIA MKATABA NA NYABUSAKAMA AMCOS, IMMACULATE RUZIKA-AFISA HABARI CPB

CPB KANDA YA ZIWA YAINGIA MKATABA NA NYABUSAKAMA AMCOS, IMMACULATE RUZIKA-AFISA HABARI CPB BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Ziwa,imeingia  mkataba wa miezi mitatu wa kununua mpunga tani 5000  kutoka kwa wakulima wa Chama cha Ushirika (AMCOS) NYABUSAKAMA cha Mkoani Geita. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CPB John Maige alipokuwa akizungumza na viongozi wa CPB na wakulima hao walipokuwa wakitia saini mkataba huo wa Mkoani hapo. Maige amesema kuwa anaamini mkataba huo utaenda kuleta matokeo chanya kwa taasisi yake pamoja na kwa Wakulima hao ambao watauza mazao yao kwa bei ya ushindani. Katika kikao  hicho Maige, aliambatana na Meneja wa CPB Kanda Ya Ziwa Alfred Kalimenze na kukutana na viongozi  NYABUSAKAMA Amcos pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Godius Kahyarara. CPB imeingia mkataba wa makubaliano  na NYABUSAKAMA Amcos  kwa ajili ya kununua Mpunga unaolimwa na wakulima waliopo kwenye Chama hicho cha Ushirika na kuuchakata katika mashine iliyopo Mkuyuni Kanda ya Ziwa Mwanza.